Matthew 12:17-21

17 aHii ilikuwa ili litimie lile neno lililonenwa kwa kinywa cha nabii Isaya kusema:

18 b“Tazama mtumishi wangu niliyemchagua,
mpendwa wangu, ninayependezwa naye.
Nitaweka Roho wangu juu yake,
naye atatangaza haki kwa mataifa.
19Hatagombana wala hatapiga kelele,
wala hakuna atakayesikia sauti yake njiani.
20Mwanzi uliopondeka hatauvunja,
na utambi unaofuka moshi hatauzima,
mpaka atakapoifanya haki ishinde.
21 cKatika Jina lake mataifa
wataweka tumaini lao.”
Copyright information for SwhNEN